Jumatatu 25 Agosti 2025 - 22:19
Rais wa Baraza Kuu la Ja‘fariyya Pakistan: Mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na Israel dhidi ya Yemen ni uvunjaji wa wazi wa sheria za kimataifa

Hawza/ Sayyid Zawar Hussein Naqawi, katika tamko lake, amelaani vikali mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya Yemen

Kwa mujibu wa idara ya tarjuma yaShirika la Habari la Hawza, Sayyid Zawar Hussein Naqawi, Rais wa Baraza Kuu la Ja‘fariyya Jammu na Kashmir Pakistan, katika tamko lake amelaani vikali mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya Yemen, na kuyataja kuwa ni uvunjaji wa wazi wa misingi na sheria za kimataifa.

Aliashiria hususan mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel dhidi ya uongozi wa juu wa majeshi ya Yemen, akiwemo Sardar Muhammad Abdulkarim al-Ghamari, ni ishara ya siasa za uvamizi na ukatili zinazofanywa na utawala huu, Ameongeza kwamba jumuiya ya kimataifa, na hasa watawala wa Kiarabu, wanapaswa kukomesha ukimya wao mbele ya jinai hizi; kwani kuendelea na mwenendo huu kutaiweka amani na uthabiti wa eneo hili katika tishio kubwa.

Sayyid Zawar Husein Naqawi, katika sehemu nyingine ya mazungumzo yake, akirejelea uvamizi endelevu wa Israel huko Yemen, Lebanon na Syria, ameusifu msimamo wa kusimama kidete na muqawama wa viongozi na wapiganaji wa Ansarullah Yemen, na akasema: ujasiri, imani na uthabiti wa wanajeshi wa Kiyemeni ni kielelezo cha wazi kwenye ulimwengu wa Kiislamu.

Aidha amesifu msimamo wa wazi wa Ansarullah katika kuwatetea watu wanyonge wa Ghaza na kusisitiza kwamba: tajiriba imeonesha kuwa utawala wa Kizayuni na washirika wake, wakiwemo Marekani na baadhi ya nguvu za Magharibi, watashindwa mbele ya azma hii ya chuma.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Ja‘fariyya Pakistan ameendelea kwa kurejelea mpango wa upanuzi wa “Israel Kubwa” na kutoa onyo kwamba: mradi huu, unaolenga kuitawala sehemu za Jordan, Syria, Lebanon, Misri, ardhi za Saudia, Iraq na hata baadhi ya maeneo ya Uturuki, ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia na unaweza kulisukuma eneo hili katika vita na uharibifu mpana.

Mwisho, amezitaka taasisi za kimataifa, mashirika ya haki za binadamu na fikra za umma za dunia zichukue mara moja msimamo wa wazi na thabiti mbele ya uvamizi huu na zichukue hatua za kivitendo ili kuzuia kuendelea kwa jinai za utawala wa Kizayuni.

Sayyid Zawar Husayn Naqawi amesisitiza kwamba: kusimama kidete kwa watu wa Yemen hakukuwa tu kumebatilisha njama za adui, bali pia kumekuwa bishara ya kushindwa utawala wa Kizayuni na wafuasi wake; na uthibiti huu unaoshuhudiwa leo Yemen ni taa yenye kung‘aa ya imani, kujitolea na subira kwa umma wa Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha